Meneja wa habari na mawasiliano Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’ amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kusimamishwa kwa kiungo wa timu hiyo James Akaminko kwasababu ya utovu wa nidhamu.
Juzi kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati yao na Yanga, timu hiyo kupitia ukurasa wa Instagram ilitoa taarifa ya wachezaji watakaoukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali ambapo kwa upande wa Akaminko ilielezwa kuwa ana adhabu.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Zaka amesema kuwa taarifa hizo si za kweli kwani wanaosambaza walitafsiri vibaya neno ‘suspended’ na kwamba kukosekana kwa mchezaji huyo kwenye mechi hiyo kulitokana na kuwa na kadi tatu za njano ambapo kikanuni hakuruhusiwa kucheza.
“Kumekuwa na taarifa mitandaoni kwamba kiungo fundi wa Azam FC, James Akaminko, amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu. Taarifa hizi siyo za kweli hata kidogo.”
“Wanaosambaza walitafsiri vibaya kutoka chapisho rasmi la Azam FC kupitia Instagram kuelekea mchezo wetu dhidi ya Yanga.”
“Kilipotajwa kikosi, yaliorodheshwa majina ya wachezaji wote, waliopo na wanaokosekana pamoja na sababu zao”.
“Kwa fundi James Akaminko pakaandikwa SUSPENDED, ni kwamba James Akaminko alisimamishwa na kanuni za ligi kutokana na kuwa na kadi tatu za njano hivyo kuukosa mchezo dhidi ya Yanga.”
Ameongeza kuwa baada ya mchezo huo, ndipo adhabu ya James ilipoishia na hivyo atakuwepo kwenye michezo mingine endapo atakuwa sawa kimwili na kiakili.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPAz
Post a Comment