Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (MwanaFA) amekabidhi kitita cha shilingi milioni 20 kwa Yanga SC baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad.
Fedha hizo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliahidi kutoa shilingi milioni tano kwa kila goli la ushindi kwenye michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
FT: Yanga SC 4-0 CR Belouizdad
Post a Comment