Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema kuwa Wachambuzi na waandishi wa soka wa Tanzania waache kuwatukana wachezaji wake pindi ambapo timu inakuwa imefanya vibaya kwani ni ngumu kwa timu kufanya vizuri kwenye michezo yote na mashindano yote kwa msimu mzima.
Gamondi amesema hayo jana Jumamosi, Februari 24, 2024 baada ya kutamatika kwa mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad na kuwafunga bao 4-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao utapigwa weekendijayo.
Ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo wa jana kutamatika, Mabingwa hao wa Algeria walikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa huo ikiwa ni pamoja na Al Ahly, Mamelodi Sundowns na Wydad Casablanca.
Ikumbukwe kuwa, katika mchezo wa kwanza kati ya timu hizi mbili uliopigwa nchini Algeria, Yanga ilinyukwa bao 3-0, lakini Wananchi hawakupoteza malengo yao ya kuitaka robo fainali.
"Rai yangu kwa waandishi wetu hapa Tanzania waache kuisema timu yangu vibaya haswa inapofanya vibaya na kuwatisha tamaa wachezaji.
"Bali wanapaswa kuwapa moyo na kutusaidia sisi walimu kutuchambua pale kwenye marekebisho kwenye kikosi kwasababu kwenye timu huwezi kuwa bora sehemu zote uwanjani," amesema Kocha Gamondi.
Post a Comment