Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele amewasilisha barua kwenye Menejiment ya klabu ya Pyramids kwaajili ya kuhitaji kusitishiwa mkataba wake.
Vyombo mbalimbali vya Habari kutoka Misri vimeripoti kuwa Mayele amedai hana furaha kuitumikia zaidi Pyramids FC na ameshafanya mazungumzo na Uongozi wake unaomsimamia ili kupata changamoto nyingine akiondoa Pyramids.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Taarifa za kuaminika ni kuwa Mayele ambaye ni raia wa Congo DR anautaka usimamizi wa Klabu ya Pyramids ya nchini Misri kusitisha mkataba wake.
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa, licha ya Simba kuonesha nia, lakini Wauza Ukwaju wa Dar es Salaam, Klabu ya Azam FC wanahusishwa pia katika mipango ya kumsajili Mayele.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment