Tano tano za Yanga zaweka rekodi hii

 Tano tano za Yanga zaweka rekodi

Wakati ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ukiifanya Yanga iandike rekodi mpya msimu huu, wachezaji wake Maxi Nzengeli na Clement Mzize wamechangia kwa kiasi kikubwa rekodi hiyo.

Mechi za CAF zote zitakuwa live kwenye app yetu bure bofya hapa KUIDOWNLOAD Ili uweze kuzitazama kupitia simu yako

Matokeo hayo ya juzi, yameifanya Yanga kuandika rekodi ya kuwa timu pekee nchini kupata ushindi wa mabao matano katika mashindano manne tofauti iliyoshiriki ndani ya msimu mmoja huku pia ikiibuka na ushindi wa idadi hiyo ya mabao mara nyingi zaidi na hadi sasa imefanya hivyo mara tano.

Hadi sasa, Yanga imefunga mabao matano katika mechi moja kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu, Kombe la Mapinduzi na ASFC.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga ilipata ushindi wa mabao 5-1 katika mechi ya hatua ya awali dhidi ya ASAS ya Djibouti, ubabe kama huo ikaufanya kwenye Ligi Kuu ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika mechi mbili tofauti dhidi ya JKT Tanzania na KMC na dhidi ya Simba ikapata ushindi wa mabao 5-1.
Asec Mimosas vs Simba bofya hapa kuzitazama mechi live

Kwenye Kombe la Mapinduzi ikaifunga Jamhuri kwa mabao 5-0 na katika mashindano ya ASFC, Yanga iliichapa Hausung ya Njombe kwa mabao 5-1 kisha juzi ikaifumua Polisi Tanzania kwa mabao 5-0.

Wachezaji ambao wanaonekana wana kismati zaidi na ushindi wa mabao matano ambao Yanga imeupata mara saba tofauti msimu huu, Maxi Nzengeli na Clement Mzize ambao wao ndio wamefunga idadi kubwa zaidi ya mabao katika mechi ambazo timu yao iliibuka na ushindi wa mabao matano ambazo kijumla Yanga imepachika mabao 35, huku ikifungwa matatu, 5-1 dhidi ya Simba, 5-1 dhidi ya Jamhuri na 5-1 dhidi ASAS ya Djibouti.


Mzize na Nzengeli kila mmoja amefunga mabao sita katika mechi saba tofauti ambazo Yanga iligawa dozi ya tano tano.
Yanga vs CR Belouizdad bofya hapa kuzitazama live

Wawili hao wanafuatiwa na Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki ambao katika mechi ambazo Yanga ilipata ushindi wa mabao matano, kila mmoja amepachika mabao matatu wakati Crispin Ngushi na Hafidh Konkoni walioondoka, Skudu Makudubela, Kennedy Musonda na Joseph Guede kila mmoja amepachika mabao mawili.

Waliofunga bao mojamoja ni Kibwana Shomari, Dickson Job, Jonas Mkude, Yao Attohoula, Mudathir Yahya, Farid Musa na Shekhan Hamis.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post