Kiungo wa Yanga, Abubakar Salum 'Sure Boy' amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi 2026.
Kiungo huyo ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2021/22 kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuachana na Azam FC aliyojiunga nayo mwaka 2007.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo kililiambia Mwanaspoti kuwa kiungo huyo ameongezwa mkataba wa miaka miwili kwaajili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo hivyo bado yupo yupo sana Jangwani.
"Ni kweli ameongezwa mkataba na viongozi hivyo mtaendelea kumuo sana kwenye viunga vya timu hii kuhusiana na makubaliano ni baina ya muajili na mwajiliwa," kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema mkataba aliopewa kiungo huyo hauna maboresho yoyote ataendelea kulipwa kama ilivyokuwa awali walivyofanya makubaliano alipokuwa anajiunga na timu hiyo.
Mwanaspoti lilifanya jitihada za kumtafuta kiungo huyo ili aweze kuzungumzia suala hilo alikiri kuongeza mkataba na timu hiyo.
"Ni kweli nimeongeza mkataba lakini sual;a la kuzungumzia ni mkataba wa muda gani nauachia uongozi maana wao ndio wenye mandeti ya kuzungumzia hilo;
"Mimi kazi yangu ni kupambana uwanjani nitazungumza kwa vitendo kulingana na namna nitakavyoipa timu matokeo mazuri uwanjani." alisema.
Kiungo huyo msimu huu amecheza mechi sita akitumika kwa dakika 331 hana bao wala asisti kwenye mashindano yote wanayoshiriki Yanga.
Post a Comment