Kocha Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amesema, moja kati ya faida kubwa waliyonayo dhidi ASEC kesho ni wachezaji wa wapinzani wao hao kutokuwa na mechi za kimashindano kwa muda mrefu.
Matola amesema, tangu mapumziko ya AFCON, ASEC hawajacheza mechi yoyote ya kiushindani kulinganisha na wao ambao tayari wamecheza mechi kadhaa za Ligi Kuu ya NBC.
"Hii ni faida kwetu sababu wapinzani wetu wameanza mazoezi kama wiki mbili zilizopita na hawajapata mechi za ushindani kama sisi hivyo hiyo ni faida kuelekea mchezo wa kesho," alisema Matola.
Simba wapo nchini Ivory Coast wakijiandaa kuwakabili ASEC hapo kesho majira ya saa 4 usiku kwa saa za hapa nyumbani Tanzania.
Post a Comment