Siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa imefika, leo ni Pacome Day ambapo timu ya Young Africans SC inakwenda kucheza mechi ya maamuzi katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad.
Taarifa iliyotolewa kupitia Yanga App inaeleza; "Tunaposema mechi ya maamuzi tunamaanisha kwamba, ushindi utakaopatikana kwa timu yetu, utaifanya kuwa na hatua chache zaidi ya kwenda kuandika historia nyingine ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
"Mchezo huo wa Kundi D utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo Jumamosi kuanzia saa 1:00 usiku, umebeba matumaini ya kufuzu robo fainali.
"Young Africans SC ikishinda leo, itafikisha pointi nane na kushikilia nafasi ya pili nyuma ya vinara Al Ahly wenye pointi tisa. Mchezo wa mwisho dhidi ya Al Ahly ugenini, tutahitaji sare tu kutimiza malengo.
"Tayari Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, amesema mchezo wa leo ni lazima kushinda, hivyo anatarajia kuona mashabiki wa Young Africans SC wakiujaza uwanja na kuisapoti timu yao
"Kutokana na hilo, ewe Mwananchi, fanya haraka kununua tiketi yako mapema ili twende uwanjani kuisapoti timu yetu.
"Mpaka sasa, tiketi za V.I.P A zilizokuwa zikiuzwa Tsh 30,00 zimemalizika sambamba na zile za Royal.
"Tiketi zilizobaki ni za V.I.P B Tsh 20,000, V.I.P C Tsh 10,000 na Mzunguko Tsh 5,000. Unaikosaje Pacome Day, twenzetu kwa Mkapa kitaalamu zaidi."
Post a Comment