Matajiri wa Dar, Azam FC wameambulia pointi moja ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons ikiwa ni mzunguko wa pili.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine umesoma Tanzania Prisons 1-1 Azam FC. Ni Samson Mbangula alianza kupachika bao mapema dakika ya 5 likawekwa usawa na Fei Toto dakika ya 54 kwa mkwaju wa penalti.
Sasa Fei anafikisha mabao 9 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni mfungaji namba moja kwa wazawa huku akiwa ni namba mbili kiujumla kwa kuwa kinara ni Aziz KI wa Yanga mwenye mabao 10 kama ilivyo jezi yake.
Kwa upande wa Tabora United jioni wamekomba pointi moja dhidi ya Singida Fountain Gate, mapema Singida Fountain Gate walipata bao kupitia kwa mshuti wa Yahya Mbegu akiwa nje ya 18, ilikuwa dakika ya 51, mwamba John Nakibinge akapachika bao akiwa ndani ya 18 kwa utulivu na header dakika ya 83.
Wakiwa wapo nyumbani wameshuhudia ubao ukisoma Geita Gold 1-3 Mashujaa kutoka mwisho wa reli Kigoma wakikomba dhahabu zote mazima.
Post a Comment