Simba inahitaji ushindi ili kutinga hatua ya makundi kuungana na Yanga ambayo tayari imefuzu na kuweka rekodi ya Tanzania kuingiza timu mbili kwenye hatua hiyo kwa msimu mmoja.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Ili kuhakikisha hilo linatokea, vigogo wa Simba wamewawekea kibunda cha maana mastaa wake ikiwa kama hamasa ya kufanya vizuri zaidi na kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Moja ya viongozi wa Simba amenieleza kuwa uongozi utatoa bonasi ya zaidi ya Sh600 milioni kwa wachezaji na bechi la ufundi kama chama hilo litashinda na kutinga robo fainali hiyo itakayokuwa ya tano kwa michuano ya CAF ndani ya misimu sita baada ya awali kuingia mara tatu kwenye ligi ya mabingwa na mara moja katika Kombe la Shirikisho Afrika.
“Unaweza kuchukulia poa lakini mechi bado ng-umu. Kuna bonasi uongozi utatoa kwa kikosi kama timu itafuzu robo fainali na kwa haraka haitakuwa chini ya Sh600 mil-ioni,” alisema kiongozi huyo.
Post a Comment