Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya pambano la Yanga SC na CR Belouizdad, mlinzi wa kati wa Yanga SC, Dickson Job amesema hamasa za kuelekea katika mchezo huo zinawaongezea kitu katika upambanaji, lakini pia zinawapa uoga.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea katika mechi hiyo, Job amesema hamasa zinazoendelea ni deni kwao wachezaji na wanatakiwa kupambana lakini kwa kufuata maelekezo ya mwalimu.
“Makocha wamefanya kazi yao kwa asilimia 100, mashabiki wanafanya kazi yao huko nje na sisi tumebakia sisi na kazi yetu ya kiwanjani.
“Hamasa zinazoendelea tunaziona na kuja muda zinatupa kitu katika mechi, lakini muda mwingine zinatupa uoga,” alisema Job.
Mechi ya Yanga itakuwa live kwenye app yetu bure bofya hapa kuidownload mapema Ili usipitwe
Job alikwenda mbali na kusema kama wachezaji wako tayari kuipambania siku ya mchezaji mwenzao (Pacome Day).
“Tuko tayari kumpambania (Pacome) katika siku yake, Nikimwangalia Pacome namuona ana ari kubwa na anaitaka mechi, kubwa ni kwamba wachezaji wote tupo tayari na tumejipanga kupata ushindi katika pambano hilo,” alisema Job.
Aidha, Job amesema kuwa hawatarudia makosa waliyoyafanya kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly ya kutaka kushambulia ili wapate mabao mengi, badala yake watacheza kwa kufuata maelekezo ya Kocha wao, Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi.
Post a Comment