Nyota wa kikosi cha Yanga SC, Maxi Nzengeli anaendelea vizuri baada ya juzi Jumamosi kupata majeraha kwenye kiganja cha mkono.
Maxi alipata majeraha hayo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa magoli 4-0 na kufuzu robo fainali ya michuano hiyo, Maxi alilazimika kutolewa kutokana na maumivu hayo, nafasi yake ikachukuliwa na Augustine Okrah.
Post a Comment