Habari Mpya kutoka Yanga ni kuhusu kipa Djigui Diarra

 Balaa la Diarra mazoezini usipime

Itazame mechi ya Yanga vs Cr Belouizdad live kupitia app yetu bure bofya hapa Sasa kuidownload bure kabisa Ili usipitwe

Kama unajiuliza juu ya ubora wa kipa wa Yanga Djigui Diarra jamaa anasumbuaje basi fika mazoezini kwao utajua jamaa ni zaidi ya kipa kwa mambo anayoyafanya huko.

Ukifika mazoezini Yanga kisha ukaangalia kwa umakini mazoezi ya kipa huyo basi utagundua kwamba jamaa habahatishi kubeba tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu Bara kwa misimu miwili mfululizo.

Diarra ana nidhamu kubwa ya kujituma mazoezini na akiwa huko mapema tu anachofanya na hata anavyopongezwa na kocha wake wa makipa Alaa El Meskini raia wa Morocco.
Yanga vs Cr Belouizdad mechi itakuwa live kwenye app yetu bure bofya hapa kuidownload

Kipa huyo mwenye "klini shiti" 6 mpaka sasa kwenye mechi 16 za timu yake za ligi amekuwa na hesabu kubwa za kupangua mashuti makali kuanzia mazoezini ambako kando ya ubora wake amekuwa akiongezewa ubora na vifaa vya kisasa vilivyopo eneo la mazoezi la timu hiyo.

Anapokuwa uwanjani mazoezini Diarra amekuwa mwepesi kujibadilisha kama mchezaji wa ndani akijaribu kuwa sehemu ya kujenga mashambulizi kwa kucheza mpira wa pasi na mabeki wake na hata wachezaji wengine huku makipa wenzake wanaomfuatia ni Aboutwalib Mshery na Metacha Mnata.

Diarra ambaye anaitumikia Yanga msimu wa tatu sasa amekuwa na ubora mkubwa wa umiliki wa mpira miguuni mwake urahisi ambao unamuondolea presha kwa mipira ya kurudishiwa.

Kitu ambacho kinamfanya ukuta wake kuwa mgumu kufungukia au kufanya makosa ni kutokana na kipa huyo kuwa makini akiwa langoni kwa kuwapanga wachezaji wake ambapo utamsikia akitumia maneno ya kiswahili kuwakumbusha wenzake kama 'anaiba' akimaanisha kuna mchezaji anavizia mpira, ruka juu, yangu au kipa akiyatumia maneno hayo kuwakumbusha kwamba anaweweza kudaka mpira huo.

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi alisema kipa huyo amekuwa bora kutokana na kuwa na juhudi kwenye kazi yake akiwa mshindani wakati wote akitamani kuona timu yake inafanya vizuri kuanzia mazoezini na mpaka kwenye mechi zao.

"Diarra ni kipa mzuri ambaye kiwango chake kimekuwa kikijieleza wazi, tuna makipa wote wazuri na bora lakini yeye kiwango chake kimejieleza kuwa chaguo la kwanza, ana juhudi na kazi yake, ni kipa mshindani ndio maana unaona anayoyafanya huku mazoezini pia utayaona kwenye mechi,"alisema Gamondi.

"Kitu kizuri zaidi tuna kocha mzuri wa makipa (El Maskini), lakini ameongezewa vifaa vingi bora vya mazoezi hii inafanya kazi kuwa rahisi unajua hili ni eneo ambalo kama huna mazoezi ya kisasa ni lazima kazi yenu itakuwa na changamoto."

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post