Baada ya kufanikiwa kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad, Wananchi wanaelekea Misri kwenda kukamilisha mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly
Yanga na Al Ahly tayari zimetinga robo fainali kutoka kundi D hivyo hii itakuwa mechi ya kuamua timu ipi inaongoza kundi
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanakwenda Misri kupambana na ikiwezekana kupata ushindi ambao utawafanya wafikishe alama 11 na kuwa vinara wa kundi
Mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyopigwa jijini Dar es salaam ilimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Mtanange huo wa kukata na shoka utapigwa Ijumaa, March 1 saa moja usiku
Jambo moja la kuweka akilini, Yanga haijawahi kuwa na 'shoo mbovu' kila ilipocheza Misri, Waarabu wajue kabisa kazi wanayo...!
Tayari timu 6 zimetinga robo fainali ambazo ni Al Ahly, Yanga, TP Mazembe, Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas na Petro Atletico
Faida ya kumaliza kinara wa kundi; katika hatua ya robo fainali ni kupangwa na timu iliyomaliza nafasi ya pili katika kundi na pia mechi ya kwanza ya robo fainali kuanzia ugenini na kumalizia mechi ya pili nyumbani
Post a Comment