“Tunawaahidi na kuwahakikishia Wanasimba kama kuna kitu kinahitajika hata kiwe kinapatikana chini ya bahari tutakifanya ili Simba iende robo fainali. Jumamosi ni kwenda kumalizia kazi.”- Meneja wa habari na mawasiliano Simba Sc, Ahmed Ally.
“Robo fainali wamefuzu watu washambawashamba sembuse sisi. Hatuwezi kushindwa kwenda robo fainali, yani waporipori wamefuzu alafu sisi wenye mashindano tushindwe? Jumamosi saa 1 usiku tunakutana kumaliza kazi.”
“Ili timu ishinde inawahitaji Wanasimba wote, sio Mo, sio Try Again, sio Mangungu bali sisi wote kwa umoja wetu. Tutawafanya Jwaneng Galaxy kitu kibaya kama ilivyokuwa kwa Horoya.”-
“Wanasimba tukiunganisha nguvu Jwaneng hawezi kutoka salama Dar es Salaam. Robo fainali zote nne zilizopita nyie ndio mmeipeleka Simba. Kama utakuja uwanjani sio tu kushangilia bali kuipeleka Simba yetu robo fainali. Mimi naamini Wanasimba tukiamua jambo letu hakuna wa kutuzia.”- Ahmed Ally.
Post a Comment