Ahmed Ally Atoa kauli ya kibabe kuelekea mechi ya Jwaneng Galaxy

Hatujawahi kushindwa mechi ya kutupeleka Robo Fainali - Ahmed Ally

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amesema, hawajwahi kushindwa mechi za kuamua hatma yao kwenda Robo Fainali.

Live Usikose kuitazama mechi ya Simba vs Galaxy live bure kwenye Simu yako download app yetu mapema Ili usipitwe bofya hapa sasa

Amewataka wanasimba kujitokeza kwa wingi Jumamosi hii Marchi 2, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kuhakikisha wanammaliza Jwaneng Galaxy kwa kuibuka na ushindi na kusonga hatua ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

“Mechi Kama hii ambayo tunakwenda kuicheza Jumamosi, Simba tumeshacheza mechi za aina hiyo tano (5) na zote tulipa ushindi.

“Hatujawahi kushindwa kupata ushindi katika mechi ya hatua kama hii ya kutupeleka hatua ya robo fainali, na Machi 2, 2024 tunaenda kuandikisha historia nyingine,” Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post