Yanga yapata wadhamini wapya wawili


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kufanya vizuri kwa klabu hiyo kuanzia uwanjani hadi kwenye utendaji wao, kumezivutia kampuni kubwa kujitokeza kufanya nao kazi


Akizungumza jijini Dar es salaam, Hersi amesema licha ya kuridhika na wadhamini walionao, kuna wengine wawili wamejitokeza kuwekeza fedha zao na hivi karibuni watawekwa hadharani


"Tunakwenda kusaini mkataba na makampuni makubwa mawili katika kipindi cha majuma mawili yajayo, yamevutiwa na utendaji kazi wetu na mafanikio yetu ya uwanjani na yanatamani kufanya kazi na sisi," alisema Hersi


Aidha, Hersi ameipongeza idara ya masoko, habari na vitengo vyote vya klabu hiyo akisema kila mmoja amefanya jukumu lake vizuri hadi kuwa kwenye mafanikio makubwa kipindi hiki


Amesema kwa sasa kuna utofauti mkubwa wa mafanikio ukilinganisha na miaka miwili iliyopita na hiyo yote ni kutokana na maboresho ambayo wamekuwa wakiyafanya kuanzia kwenye benchi la ufundi, wachezaji na idara zote

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post