Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mkataba huo wa miaka mitatu una thamani ya Tsh Milioni 900
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mkataba huo matokeo mazuri ya uhusiano kati ya Yanga na NIC akiamini utawapa fursa wachezaji wa Yanga kutuzwa katika kila mwezi
"Mkataba huu ni wamiaka mitatu na thamani yake itakuwa milioni 900. Mkataba huu utakuwa unalenga moja kwa moja kwa mchezaji bora wa mwezi,tunakuhakikishia mkataba huu utakupa thamani sahihi ya kile ulichokiwekeza kwetu"
"Kwetu sisi kama Yanga Sc ni heshima kubwa sana kufanya kazi na kampuni kubwa kama hii kutokana na utendaji wetu sahihi ndani ya klabu yetu"
"Tunakuakikishia ushirikiano mkubwa sana toka kwetu na tunakuakikishia tutakwenda mbali zaidi ya hapo sisi na kampuni yako," alisema Hersi
Tuzo ya mchezaji bora itaanza mwezi huu Oktoba ambapo mwanzoni mwa mwezi Novemba wachezaji watatu waliofanya vizuri Oktoba watapigiwa kura na mashabiki ili kumpata mshindi
Post a Comment