Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya ligi kusimama kupisha kalenda ya FIFA, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapa wachezaji wake mapumziko ya siku chache kabla ya kurejea kuendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu utakaofuata
Oktoba 25 Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kumenyana na Azam Fc katika mchezo ambao alama tatu kwa Yanga zitawarejesha kileleni mwa msimamo wa ligi
Aidha wachezaji walioitwa kwa ajili ya majukumu ya timu za Taifa, wao wameelekea katika Mataifa yao
Wachezaji 10 wa Yanga wameitwa katika timu za Taifa. Wachezaji hao ni Djigui Diarra, Metacha Mnata, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Nickson Kibabage
Wengine ni Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki na Clement Mzize
Post a Comment