Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Simba leo imetangaza viingilio vya mchezo wa robo fainali African Football League kati ya Simba dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa Oktoba 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Ahmed Ally, amesema wameweka viingilio rafiki ili kuhakikisha wanasimba wanajitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo huo unaozikutanisha timu kubwa kwenye mashindano makubwa zaidi barani Afrika
Ahmed amewataka Wanasimba kununua tiketi zao mapema ili kuwa sehemu ya historia ambayo inakwenda kuandikwa uwanja wa Benjamin Mkapa mbele ya Rais wa FIFA, Giani Infantino
"Ni tukio jipya duniani, Afrika na hata Tanzania. Ni tukio pekee lenye thamani zaidi ndani ya wiki hizi mbili barani Afrika. Hii ndio michuano mikubwa zaidi barani Afrika na inashirikisha watu bora pekee na watu bora Tanzania ni Simba Sc"
"Halijaja kwa bahati mbaya, ni kwa juhudi ambayo Simba imeifanya. Wakati wanapanga timu za kushiriki waliangalia timu zenye thamani na ubora. Kwanini Simba Sports Club ni sababu ya ubora wetu. Kila Mtanzania aseme asanteni na hongera Simba Sc"
"Hili sio jambo la kawaida na sio tu mchezo lakini ni ufunguzi wa michuano hii. Hili ni jambo kubwa zaidi kutokea kwenye historia ya mpira wa miguu Tanzania. Hii ni African Football League ya kwanza duniani, mwakani na miaka ijayo timu zitaongezeka zaidi ya nane hivyo thamani yake haitakuwa sawa na sasa. Ni aibu siku hiyo uwanja ukiwa haujaa. Sio siku ya mtu kukosa."
"Viingilio tumepanga kwa kuangalia hali za watu wetu. Platinum - Tsh. 200,000 VIP B- Tsh. 40,000 VIP C - Tsh. 30,000 Machungwa - Tsh. 10,000 Mzunguko - Tsh. 7,000. Hatutakuwa na VIP A sababu jukwaa limechukuliwa na FIFA na CAF," alisema Ahmed
Ahmed amesema itafanyika kampeni kubwa ya hamasa kuanzia sasa mpaka siku ya mchezo ambapo watazunguuka jiji zima la Dar es salaam kuwahamasisha Wanasimba kuja uwanjani kuipa sapoti timu yao katika mchezo ambao wanahitaji ushindi
"Tutazunguka Dar nzima kufanya hamasa. Tarehe 14 ndio tutazindua wiki ya Kispika (Wiki ya Hamasa), tutazindulia Coco Beach. Kutakuwa na matukio mbalimbali kama mechi za mashabiki na pia kutakuwa na watu wa kuuza tiketi, watu wa NMB na CRDB kwa ajili ya watu kupata namba za mashabiki lakini pia jezi zitauzwa pale"
"Mechi itachezwa saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa ambao na Simba imechangia ukarabati wake hivyo wajue wakicheza kwenye uwanja ule wanacheza sehemu ambayo Simba imechangia ukarabati," alitamba Ahmed
Post a Comment