Taifa Stars yatupwa kundi la kifo AFCON2023

 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Tanzania imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast.


Katika droo iliyopangwa usiku huu Jijini Abidjan, Kundi A lina wenyeji Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea-Buissau.


Kundi B linaundwa na Misri, Ghana, Cape Verde na Msumbiji, wakati Kundi C lina Senegal, Cameroon, Guinea na The Gambia.


Kundi G linazikutanisha Algeria, Burkina Faso, Mauritania na Angola wakati E kuna Tunisia, Mali, Afrika Kusini na Namibia.


Fainali hizo zinatarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024, hii ikiwa mara ya tatu kwa Tanzania kushiriki Kihistoria baada ya 1980 Nigeria na 2019 Misri.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post