Taifa Stars kuanza na Morocco AFCON 2023

Taifa Stars kuanza na Morocco AFCON 2023

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Timu ya taifa ‘Taifa Stars’ itafungua Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika Ivory Coast mwakani kwa kucheza na Morocco, Januari 17 katika Uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro.


Mchezo huo utafungua mechi za kundi F lililo pia na Zambia na DR Congo na umepangwa kuanza saa 2:00 usiku.


Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) juzi jioni, mchezo wa pili wa Stars utakuwa Januari 21 dhidi ya Zambia na itahitimisha hatua ya makundi na DR Congo Januari 24.


Stars imekuwa haina historia nzuri na mechi ya kwanza ya makundi katika fainali za Afcon ambapo mara mbili ilizoshiriki ilipoteza mechi ya ufunguzi.


Mara ya kwanza ilikuwa 1980 zilipofanyika Nigeria ambapo ilipoteza mechi ya kwanza ya kundi kwa mabao 3-1 kutoka kwa Nigeria. Pia mechi ya kwanza ya makundi ilipoteza 2019 zilipofanyika Misri dhidi ya Senegal kwa mabao 2-0.


Lakini dhidi ya Morocco, Stars sio tu itakuwa inasaka historia ya ushindi katika mechi ya kwanza ya kundi, bali itakuwa ikitafuta ushindi wa kwanza wa fainali za Afcon kwani haikuwahi kushinda mchezo wowote.


Katika mara mbili ambazo imeshiriki imecheza mechi sita za makundi, imetoka sare moja tu huku ikifungwa michezo mitano.


Kocha msaidizi wa Stars, Hemed Morocco alisema hawana hofu kwa ratiba hiyo na wanachokifikiria ni kujiandaa vizuri ili waandike historia katika Afcon mwakani.


“Makundi yakishapangwa maana yake utacheza dhidi ya kila timu ambayo ipo kwenye kundi jambo ambalo hata sisi tulishajiandaa nalo. Kinachohitajika ni maandalizi ya uhakika ambayo yatatuwezesha kupata matokeo mazuri katika mechi zote tatu za kundi ili tuingie katika hatua inayofuata,” alisema.


Chanzo: Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post