Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Musonda alianza vyema msimu kabla ya kupata majeraha ambayo yamemfanya aingie na kutoka kikosini kwa nyakati tofauti
Yanga imethibitisha kuwa Musonda amepona kwa asilimia 100, Farid Mussa akiwa mchezaji pekee ambaye anaendelea kuimarika kutoka kwenye majeraha
Unaweza kusema mshambuliaji huyo kutoka Zambia bado ana deni kubwa kutoka Wananchi kwani baada ya kuondoka Fiston Mayele, wengi walitarajia yeye kuwa ndiye mshambuliaji kiongozi
Badala yake kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amekuwa akimtumia kinda Clement Mzize zaidi Musonda akikosekana baadhi ya mechi akiwa majeruhi
Jumapili ya wiki hii Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex kumenyana na Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Musonda ana kumbukumbu nzuri mbele ya Azam Fc, msimu uliopita alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) mchezo ukipigwa uwanja wa Mkwakwani
Pengine hii ni mechi ambayo Musonda anaweza kuitumia kurejesha kasi yake ya kuzifumania nyavu. Katika msimu huu Musonda amefunga bao moja tu kwenye ligi kuu ya NBC
Post a Comment