Simba yawaita mezani Saido, Aubin Kramo

 Simba yawaita mezani Saido, Aubin Kramo

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Uongozi wa Simba umekaa kikao na kuazimia kuwaita mezani baadhi ya wachezaji wake wakiongozwa na washambuliaji aidi Ntibanzokiza 'Saido' na Aubin Kramo ili kujadili mikataba yao.


Simba inataka kumwongezea Saido mkataba kabla haijafika Desemba ili kumdhibiti kuondoka kikosini hapo kwani mkataba wake wa awali (wa mwaka mmoja), aliousaini kwenye dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Geita Gold utamalizika Desemba.


Mwananchi linafahamu tayari Saido na Simba wameanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na kila pande imewasilisha matakwa yake na mchakato wa majadiliano unaendelea vizuri.


Wakati Saido akiwa mbioni kusaini mkataba mpya, hali iko tofauti kwa Kramo, ambaye mabosi wa Simba wanapiga hesabu za kuachana naye kwenye dilisha dogo, Januari, kutokana na kuandamwa na majeraha yanayomweka nje kwa muda mrefu.


Tangu alipojiunga na Wekundu wa Msimbazi, mwanzoni mwa msimu huu akitokea Asec Mimosas ya nchini kwao Ivoey Coast, kiungo huyo mshambuliaji hajacheza katika mechi yoyote ya kimashindano.


Kramo yuko nchini kwao akilikokwenda kwa matibabu, lakini imeelezwa viongozi wa Simba wapo tayari kufungua mazungumzo ya kuvunja mkataba ili kupata nafasi ya kusajili mchezaji mwingine na imepanga kushusha beki wa kimataifa.


Chanzo: Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post