Simba waombe nyota wao wasiende timu za Taifa - Kiemba

Simba waombe nyota wao wasiende timu za Taifa

 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kuelekea maandalizi ya mchezo wa ufunguzi wa African Football Legue [Simba vs Al Ahly] huenda Simba ikawakosa nyota kadhaa endapo wataitwa na kwenye timu zao za Taifa katika kipindi hiki cha kalenda ya FIFA.


Mkongwe Amri Kiemba amesema, anafikiri ni muhimu Simba ikatuma maombi kwa mashirikisho ya soka ya nchi za wachezaji wake ili wabaki na wachezaji katika kipindi hiki wakati wanajiandaa na mchezo huo mkubwa.


“Mimi nadhani wachezaji wa Simba si lazima wawepo timu ya Taifa [Taifa Stars] kwa sababu Simba ina mechi ngumu ya mashindano [Simba vs Al Ahly] lakini Taifa Stars ina mechi ya kirafiki.”


“Kwa timu za taifa za mataifa mengine [DR Congo, Zambia, n.k] Simba wanaweza kuomba wachezaji wao waendelee kubaki klabuni kujiandaa na mechi ya ufunguzi wa African Football League.”


“Kwa sababu kuna wachezaji wengine wanaitwa timu za Taifa na hawapati nafasi ya kucheza, wanaishia kukaa tu benchi na wengine hata kwenye benchi hawakai.”

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post