Robertinho awekwa mtu kati Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Robertinho awekwa mtu kati Simba


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Licha ya kufanikiwa kuivusha Simba hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira yuko katika presha kubwa


Baada ya mchezo dhidi ya Power Dynamos uliopigwa uwanja wa Azam Complex jana na Simba kulazimishwa sare ya bao 1-1 matokeo ambayo yalitosha kuwapeleka Wekundu wa Msimbazi makundi kwa faida ya mabao mawili waliyofunga ugenini, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba ilikutana kwa dharura kujadili kile kilichoelezwa kutoridhishwa na kiwango cha timu


Msimu huu mashabiki wa Simba wametoa malalamiko karibu kila baada ya mechi kutoridhishwa na kiwango cha timu yao licha ya kupata matokeo mazuri         


Hofu iliyopo ni kwamba hakuna uhakika kama Simba itaweza kufikia malengo yake ya kushinda nataji yote ya ndani pamoja na kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa kama timu itaendelea kucheza kama ilivyo sasa


Miongoni mwa waliotoa malalamiko ni Rais wa heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ambaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii aliandika ujumbe unaoashiria haridhishwi na kile alichokishuhudia


Katika misimu iliyopita, Simba ilidumisha utamaduni wake wa kucheza kandanda safi iliyoambatana na ushindi na zaidi kwenye michuano ya Kimataifa Simba imejijengea heshima ya kuwa timu hatari sana inapocheza mbele na mashabiki wake


Robertinho amekuja na falsafa tofauti ambapo jambo muhimu kwake ni timu kupata matokeo mazuri pasipo kujali wamecheza vipi


Mpaka sasa Robertinho amefanikiwa katika mbinu zake, hajapoteza mchezo katika mechi tisa zilizopita


Mwanzoni mwa msimu huu aliiongoza Simba kutwaa Ngao ya Jamii na ameweza kushinda mechi zote tatu katika ligi kuu pamoja na kuipeleka Simba hatua ya makundi CAF CL


Hata hivyo presha ya mashabiki ambao hawaridhishwi na vile timu yao inacheza, imepata nguvu zaidi baada ya kuanza kuungwa mkono na baadhi ya viongozi


Pengine Robertinho na benchi lake la ufundi wanapaswa kufanya kitu haraka kwa kuanzia mechi inayofuata kwenye ligi kuu dhidi ya Prisons itakayopigwa Alhamisi huko Mbeya


Baada ya mechi hiyo Simba inakabiliwa na mechi mbili za AFL dhidi ya Al Ahly, mchezo wa kwanza ukipigwa Oktoba 22 uwanja wa Benjamin Mkapa na marudiano kupigwa Oktoba 24 huko Misri



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz