Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Uongozi wa Simba ulifanya jitihada za kuomba wachezaji hao wabaki kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa African Football League dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Ijumaa ijayo Oktoba 20, ni wazi imeshindikana
Wachezaji hao ni Henock Inonga ambaye yupo na timu ya taifa ya DR Congo iliyoweka kambi New Zealand, Clatous Chama yupo Misri na kikosi cha timu ya taifa ya Zambia, Kibu Dennis, Mzamiru Yassin na Ally Salim hawa wapo kwenye kikosi cha Stars kilichosafiri leo UAE
Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan itakayochezwa Saudi Arabia Oktoba 15
Taarifa kuoka Misri zimebanisha kuwa wapinzani wa Simba Al Ahly wao wamefanikiwa kuwazuia wachezaji wao wote walioitwa timu za Taifa ili kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba
Al Ahly wanatarajiwa kutua nchini Oktoba 17 kwa ajili ya mchezo huo
Post a Comment