Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba iliyojiwekea malengo ya kucheza nusu fainali katika msimu huu, imepangwa kundi B pamoja na Jwaneng Galaxy, Asec Mimosas na Wydad Athletic
Habari njema zaidi kwa Simba ni kuwa mechi ya kwanza katika hatua ya makundi watacheza nyumbani na pia mechi ya mwisho watamaliza nyumbani
Asec Mimosas watakuwa wa kwanza kuvuta pumzi ya moto katika uwanja wa Benjamin Mkapa, mchezo ukitarajiwa kupigwa Novemba 24-26 2023
Baada ya mchezo huo Simba itasafiri Botswana kuikabili Jwaneng Galaxy Disemba 01-02 kisha kuelekea Morocco kuikabili Wydad Athletic Disemba 08-09
Disemba 19 Wydad atakuja Tanzania kuvuta pumzi ya moto kabla ya Simba kusafiri Ivory Coast kuikabili Asec Mimosas February 23-24
Hesabu za makundi zitafungwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa March 01-02 kwa mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy
Hii inaweza kuwa mechi ya kuipeleka Simba robo fainali na hakuna shaka itakuwa mechi ya kisasi pia kwa hawa 'Makiri-kiri'
Post a Comment