Mo Dewji aweka Sh1 bilioni mezani, vigogo watangulia Misri

Mo Dewji aweka Sh1 bilioni mezani, vigogo watangulia Misri

 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Tajiri na mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ na jopo lake, wamewawekea mezaji wachezaji Sh1 bilioni ili waitoe Al Ahly kwenye michuano ya Africa Football League.


Katika michuano hiyo iliyozinduliwa Dar es Salaam jana jioni ikihusisha mastaa kibao akiwemo Kocha Arsene Wenger, Mo amewaambia pia kama wakimfurahisha zaidi kwa kumheshimisha anaweza kupandwa mzuka na kufanya kufuru zaidi.


Simba inarudiana na Ahly Jumanne jijini Cairo, Misri ambapo kwa kushiriki michuano hiyo tayari kama klabu wana uhakika wa Sh2.5 bilioni.


Kwenye kikao na wachezaji jijini Dar es Salaam juzi usiku, Mo aliwaambia kwamba mechi ya jana endapo wangeshinda angetoa Sh500 milioni na ile marudiano atafanya vivyohivyo.


Kauli hiyo iliwapandisha mzuka wachezaji ambao kwa wiki hii nzima walikuwa wakisubiri kauli ya tajiri na bodi yake, kwani wao tayari walikuwa wakiendelea na yao mazoezini na kambini.


Simba wamepania kufanya makubwa kwenye mechi ya marudiano kwani wanaamini haijaisha mpaka iishe na wanasaka heshima kuendeleza vaibu la jana usiku Kwa Mkapa.


Katika michuano hiyo ya muda mfupi yenye fedha nyingi, ili kutwaa kombe kila timu italazimika kucheza mechi sita za kivumbi na jasho kama kile cha jana usiku. Bingwa anabeba Sh10 bilioni, mshindi wa pili Sh7.5 bilioni na kucheza nusu fainali Sh4.3 bilioni.


VIGOGO WATUA CAIRO


Mwanaspoti linajua kwamba tayari Simba imetanguliza vigogo wawili nchini Misri kuweka mambo sawa na moto utakuwa ni uleule waliokuja nao Ahly Dar es Salaam.


Simba wamepania kubeba asilimia kubwa ya vitu vyao kama walivyokuja navyo Ahly ingawa hata viongozi waliopo Misri tayari wameshafanikisha mahitaji kadhaa kuhakikisha timu inatua kishua.


Kitakwimu, Simba ndio klabu ya Tanzania na Afrika Mashariki yenye uzoefu mkubwa si tu na timu za Misri, bali majiji makubwa ya nchi hiyo kwani imecheza na kuweka kambi mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni.


Simba ndiyo klabu pekee ya Cecafa inayoshiriki michuano hii ya timu nane, kigezo kikiwa ni ubora kwenye viwango pamoja na kuwa na ushiriki wa mara kwa mara kufikia hatua ya robo fainali.


Chanzo: Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post