Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ufunguzi wa AFL siku ya Ijumaa ndio gumzo kubwa kwenye mitandai ya kijamii, mchezo kati ya Simba dhidi ya Al Ahly ukitarajiwa kupigwa siku hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika
Try Again amesema mwekezaji wa Simba ambaye ni Rais wa heshima Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ameahidi bonus kubwa kwa wachezaji kama watapata ushindi dhidi ya Al Ahly na kuwaondosha wababe hao katika mashindano ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika
"Inaeleweka Mwekezaji wetu Mo Dewji hana masihara zinapokuja mechi za mashindano makubwa. Kuna fungu kubwa limetengwa kwa ajili ya wachezaji ili kuhakikisha wanashinda mchezo dhidi ya Al Ahly"
"Siwezi kusema ni kiasi gani lakini wachezaji wanafahamu ni pesa nyingi kwelikweli. Unajua masuala haya ya fedha huwezi kutangaza hadharani ili kuwaepushia wachezaji usumbufu usio wa lazima," alisema Try Again
Mpaka sasa Simba ina uhakika wa kuvuna Tsh Bilioni 2.5 kutokana na ushiriki wake katika michuano hiyo inayokutanisha vigogo nane kutoka kila kanda barani Afrika
Post a Comment