Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ni Ricardo Ferreira kutoka nchini Brazil mbinu zake zitaanza kutumika ndani ya kikosi cha Singida Fountain Gate kwenye kusaka ushindi.
Mkataba wake ni wa mwaka mmoja kuwanoa mastaa wa Singida Fountain Gate inayoshiriki Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere, Beno Kakolanya, Bruno Gomes.
Yupo na msaidizi wake ambaye ni Andrew Barbosa hawa watafanya kazi kwa kushirikiana ndani ya timu hiyo.
Ni mikoba ya Ernst Middendrop alikuwa kocha wa timu hiyo akawaga manyanga mazima baada ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Ricardo ana rekodi ya kufundisha klabu kubwa barani Afrika kwa mafanikio zikiwemo Al Hilal, Al Merrikh SC na Ismaily SC.
Post a Comment