Mazembe, Esperance kukutana Kwa Mkapa

 Mazembe, Esperance kukutana Kwa Mkapa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mchezo wa Africa Football League kati ya TP Mazembe ya DR Congo na Esperance de Tunis ya Tunisia uliokuwa ufanyike kwenye uwanja TP Mazembe, jijini Lubumbashi umehamishwa na sasa utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.


Mchezo huo ambao ulipangwa kupigwa Oktoba 22 wa mkondo wa kwanza umehamishwa baada ya serikali ya Congo kuzuia vifaa vya kurushia matangazo ya mchezo huo kuingia nchini humo. Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa Uwanja wa Hammadi Agrebi Oktoba 25, Tunisia.


Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana kwenye michuano hii ambayo imeanzishwa mwaka huu ikizihusisha timu nane.


Mbali ya mechi hii, uwanja wa Mkapa utatumika kwa ajili ya mechi ya ufunguzi na Simba itakipiga dhidi ya Al Ahly ya Misri. Esperance ilithibitisha suala hili la mechi yao kucheza kwa Mkapa kupitia tovuti yao rasmi.


Pia kuna tetesi huenda Al Hilal ikachagua uwanja wa Mkapa kwa ajili ya kucheza mechi zao za hatua ya makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post