Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amekiri kuwa mchezaji mwenzake katika nafasi hiyo Yao Kouassi anampa darasa
Tangu atue Yanga katika dirisha la usajili lililopita, Yao amejihakikishia nafasi mbele ya Kibwana ambaye katika misimu miwili iliyopita alitumika kwenye 'mbavu' zote
Kibwana amesema Yao anaonyesha uwezo mkubwa, kuna vitu vingi anafanya uwanjani ambavyo nae anaweza kuviiga ili kuwa bora zaidi
"Ni kweli sasa sipati nafasi, nakubali kuzidiwa uwezo na Yao. Ni mchezaji mzuri ambaye ana uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia"
"Ana pumzi akipanda anawahi kurudi kuzuia mashambulizi na ana nguvu. Hilo limeniamsha na kunipa akili ya kuongeza ujuzi zaidi ili nirudi kwenye ushindani"
"Bado nina nafasi ya kucheza na nitafanya kwa ubora ili kumpa imani kocha kuwa hakosei kunipa nafasi ya kucheza," alisema Kibwana
Yao ndio kinara kutoa pasi za mabao kwenye ligi kuu ya NBC akitoa pasi tatu huku pia akiwa amefunga bao moja
Post a Comment