Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe usiku wa kuamkia leo amelazimika kwenda Chang’ombe Temeke Jijini Dar es salaam katika ghala la Toshi Logistics lililohifadhi shehena ya jezi feki za Simba, Yanga na Taifa Stars baada ya kusikia mzigo huo unataka kutoroshwa.
Ally akiwa ameambatana na Waandishi wa habari ameiomba Serikali iingilie kati suala hilo ili haki itendeke kwani mzigo uliokamatwa untajwa kuwa na thamani ya mabilioni.
Wakati Ally alipofika eneo la tukio Mlinzi wa eneo hilo alianza kuleta vitisho vya kutaka kumpiga kabla ya baadhi ya Watu kumzuia, inasemekana inafanyika njama ya kuondoa mzigo huo.
"Utuibie halafu ututishie kutupiga na chuma? Sisi wote hapa ni wanaume, hatuogopi kitu. Mbona unatuzuia? Embu nipige na hiyo chuma tuone! Wewe vipi, unanyanyua chuma? Hawa watu hawana hata woga, hii nchi unaiongoza wewe?
"Hii vita ni kubwa ndugu zangu, lazima tuwe macho tuunganishe nguvu kuwadhibiti watu kama hawa. Watu wachache ambao kwa maslahi yao wanaumiza mamilioni ya Watanzania. Hawajui madhara ya kudhulumu vilabu vyetu na timu yetu ya Taifa na kuidhulumu Serikali kodi yake," amesema Kamwe.
Itakumbukwa juzi Mwakilishi wa Kampuni ya GSM kwenye msako uliozikamata jezi hizo feli alisema iwapo jezi hizo za Yanga pekee zingeingia sokoni zingeisababishia Kampuni hiyo hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 2.
Akizungumza katika tukio hilo, Kamwe amesema; “Huyu mtu ametengeneza mzigo mubwa ambao ni feki, ametumia nembo ya Yanga bila ridhaa yetu, hana hata hofu, hajui kama hivi vilabu vimeshikilia mioyo ya watu. Hawa ni watu wabaya na hawana nia njema hata kidogo kwenye nchi yetu. Tunapaswa kuwakemea na Serikali iwakemee.
“Walioingiza huu mzigo wanapaswa wawe mfano kwa wengine kwamba hili jambo ni baya na halikubaliki, sio tu kuhujumu maendeleo ya klabu bali unahujumu Taifa letu kwani linakosa mapato.
“Inapotokea mtu anataka kurudisha nyuma jitihada za Rais Samia Suluhu kulisogeza mbele gurudumu la soka letu, anapaswa akemewe,” amesema Kamwe.
Post a Comment