Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ahmed na timu ya hamasa leo wako mitaa ya Manzese Bakhresa wakitoa hamasa kuelekea mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Ijumaa Oktoba 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ahmed amesema Wanasimba wana kila sababu ya kutamba kwani wiki hii ni yao, sio kwa bahati wao kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa timu nane zinazoshiriki AFL, bali ni kutokana na mafanikio ya timu yao
"Kuna jambo kubwa Afrika hii ambalo ni AFL linaihusisha Simba na Al Ahly. Ni heshima kubwa Simba tumepewa kuandaa mechi ya ufunguzi wa mashindano haya kwa mara ya kwanza"
"Wengine wataishi maisha ya shida sana wiki hii, na sisi sio shida zetu tutazidisha dozi.Tumepewa wenyeji wa michuano hii sababu ya ubora ambao tupo nao, zipo timu nyingi Tanzania, zipo timu nyingi Afrika lakini walikaa kujadili timu gani inafaa wakaona Simba Sports Club."
"Hatujapata nafasi hii kwa bahati mbaya, tumepata kwa ubora tulionao. Kama sio Simba kuwepo Tanzania basi Tanzania kusingekuwa na timu inayoshiriki African Football League kwa sababu baada ya Simba hakuna mwingine mwenye mafanikio kimataifa zaidi yetu"
"Ukweli unabaki kuwa sisi Wenye Nchi ndio tumeleta AFL hapa. Wanasimba mna nafasi kubwa ya kujipongeza, kufurahi sababu tumekomboa nchi kupata nafasi ya michuano hii, na kwenda mbali zaidi ya kuwa mwenyeji wa michuano," alisema Ahmed
Ahmed amewataka Wanamsimbazi kutumia fursa hii ya kihistoria kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo ambao wamejiandaa kushinda
"Hii ndio michuano yenye thamani zaidi barani Afrika na wenye michuano wakasema timu inayofanana na michuano hii Tanzania ni Simba Sports Club"
"Watu wanafanya kazi mchana na usiku sababu yetu, wanaandaa Uwanja wa Mkapa kwa ajili yetu, viti vinaoshwa na maji na sabuni sababu yetu, wakaulizwa kwa nini mnasafisha na maji na sabuni wakasema sababu wanakuja kukaa mashabiki wa Simba, Wanalunyasi"
"Maandalizi haya babkubwa yanayofanyika yanatuhitaji kwenda uwanjani. Hakuna Mwanasimba anatakiwa kubaki nyumbani, hiyo siku ni kwenda uwanjani. Historia hiyo itabaki kwa vizazi na vizazi."
"Lazima tuambiane ukweli AFL ya safari hii imeshirikisha timu nane bora na Mnyama yupo kati ya timu hizo bora, AFL zijazo zitakusanya kila mtu ambayo haitakuwa na thamani sawa na hii ya kwanza"
Post a Comment