Haji Manara akomalia bao la Singida FG, adai Simba wanabebwa

 Manara aibuka na bao la Singida, adai Simba wanabebwa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa jana pale CCM Liti, mkoani Singida ulimalizika kwa Simba Sc kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Singida Fountain Gate FC.


Baada ya mchezo huo kumalizika, mjadala ukaibuka kuwa bao la Elvis Rupia wa Singida lilikuwa bao halali na haikuwa offside kama ambavyo mwamuzi Tatu Malogo aliamua.


Ofisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ameona asikae kimya, amemaua kufunguka na kuwalaumu waamuzi kwa kuharibu mchezo huo huku akidai kuwa polepole sasa SImba anakusanya alama za dhulma hivyo anaweza kunyakua ubingwa kama masihara.


"Goli halali linakataliwa kisha Wanaenda kupewa clear offside bila haya wala aibu. Imagine kati ya mechi tano walizocheza tatu ni maumivu kwa wapinzani wao. Wataendelea kukusanya points za dhulma na tukija kustuka ubingwa huo hapo kwao.


"Lazma tuseme kwa nguvu bila kumuonea mtu haya,tuiambie Mamlaka wazi wazi kuhusu ubabaifu uliokithiri wa udhalimu unaoendelea na tusijali matokeo ya adhabu zao, maana tutakuwa tunataka haki ya ligi bora isiyo na dhulma," amesema Manara.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post