Droo ya Makundi Afcon 2023 kupangwa Leo

 Taifa Stars kujijua leo AFCON 2023

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars, leo itafahamu wapinzani wake watatu katika kundi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika mwakani huko Ivory Coast baada ya droo itakayochezeshwa Abidjan,nchini humo kuanzia saa 3 usiku.


Kwenye droo hiyo itakayoongozwa na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Tanzania itakuwa katika chungu cha nne pamoja na Guinea Bissau, Msumbiji, Namibia, Angola na Gambia.


Kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa na CAF uchezeshaji wa droo hiyo kutakuwa na makundi sita yatakayoundwa na timu nne, moja kutoka kila chungu kati ya vinne vitakavyokuwa na timu sita kila kimoja kulingana na nafasi ambayo ipo katika viwango vya ubora.


Timu mwenyeji, Ivory Cosat itapangwa kundi A na hivyo inasubiri nyingine tatu kutoka katika chungu namba mbili, tatu na nne. Kitendo cha Tanzania kuwekwa katika chungu cha nne kinaiweka katika uwezekano wa kupangwa kundi gumu kutokana na ubora wa vikosi na wachezaji wa timu zilizopo katika vyungu vitatu tofauti na ambacho Taifa Stars ipo.


Chungu cha kwanza ambacho timu inayoweza kupangwa na Stars kina Ivory Coast, Morocco, Senegal, Tunisia, Algeria na Misri wakati cha pili kina Nigeria, Cameroon, Mali, Burkina Faso, Ghana, na DR Cong.


Chungu cha tatu kina Afrika Kusini, Cape Verde, Guinea, Zambia, Guinea ya Ikweta na Mauritani.


Mkurugenzi wa ufundi wa TFF, Oscar Milambo aliliambia gazeti hili kuwa Taifa Stars ipo tayari kupangwa na timu yoyote katika fainali hizo na inasubiri kwa hamu kujua itapangwa na nani.


“Tunaisubiri droo kuona tutapangwa na nani lakini jambo la msingi ni kufanya maandalizi ambayo yatatufanya tuwe tayari kukabiliana na mataifa ambayo yameshajipambanua kuwa ni makubwa kisoka.”

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post