Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Sokoine
Akizugumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Robertinho alisema wanatambua ugumu wa mchezo huo kwani mechi za nyuma walizocheza katika uwanja wa Sokoine dhidi ya Prisons hazijawahi kuwa rahisi
"Nashukuru tumefika salama hapa Mbeya na tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons hapo kesho"
"Tunawaheshimu Prisons kwani nakumbuka msimu uliopita walitupa mechi ngumu lakini wakati huu tumejipanga"
"Tumejipanga kucheza soka la ushindani kuwapa burudani mashabiki wetu na kushinda mchezo huu," alisema Robertinho
Simba ilitua mkoani Mbeya jana na leo inatarajiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Sokoine
Katika mchezo huo Simba itawakosa wachezaji wake watatu, Hennock Inonga, Aubin Kramo na mlinda lango Aishi Manula ambaye bado anaendelea kuimarika baada ya kuwa nje kwa muda mrefu
Post a Comment