Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Highland Estates, Mbarali Mbeya, Gamondi alibadili takribani wachezaji saba walioanza katika mchezo uliopita kwenye ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh
"Tumepoteza mchezo sio kwa sababu nimefanya mabadiliko ya kikosi, tumefungwa kwa sababu tulifanya makosa"
"Nafikiri bao la kwanza tuliwapa zawadi, tulizungumza mapema kuwa uwanja haukuwa rafiki kwetu hivyo tuepuke kucheza kwenye eneo letu lakini yakafanyika makosa ambayo yalipelekea tukafungwa"
"Bao la pili lilikuwa shambulizi la kushitukiza, hatukufanya vile ambavyo tulipaswa kufanya na kupelekea tukaadhibiwa"
"Kama tungepata ushindi leo hakuna mtu angezungumzia mabadiliko. Wakati mwingine ni muhimu kufanya mabadiliko haya kwa kuzingatia ratiba inayotukabili," alisema Gamondi
Gamondi aliongeza kuwa haukuwa mchezo wa kuvutia hasa kwenye kipindi cha pili pale Ihefu Fc walipoamua mpira usichezwe na waamuzi kuacha kuchukua hatua
"Sisi tumepoteza mechi uwanjani lakini kulikuwa na matukio mengine sana yasiyo ya kimichezo inasikitisha kuona hakuna hatua zilizochukuliwa," alisema
Post a Comment