Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya Yanga kupangwa kundi “D” ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ikiwa na Al Ahly, Belouizdad na Medeama Afisa Habari Yanga, Ally Kamwe ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ya kwamba.
"Kundi D hakuna ubishi, hili ni Kundi Dume kweli, yupo Bingwa mtetezi, Al Ahly, yuko Belouizdad kutoka Algeria, yuko pia Medeama kutoka Ghana.
"Nini msimamo wetu kama Yanga sc? Hii ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuipima project yetu ya michuano ya Kimataifa.
"Ni nafasi nzuri kwetu kuipima quality ya kikosi chetu dhidi ya Timu zenye Quality kubwa. Ni nafasi nzuri sana kwetu Yanga kwenda kuitangaza vyema Klabu yetu kwenye michuano ya Kimataifa.
"Siri yetu ya mafanikio ni ileile, kuungana na kushikamana kwa pamoja kama Taasisi. Kila mtu akicheza vyema kwenye Nafasi yake, INAWEZEKANA Daima Mbele Nyuma Mwiko," ameandika Ally Kamwe.
Post a Comment