Alichokisema Ahmed Ally baada ya Simba kufuzu hatua ya makundi kwa tabu

 Tunasikitika kumpoteza mpinzani halisi Power Dynamos - Ahmed Ally

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amekiri kupata tabu katika safari ya kusaka tiketi ya kucheza Hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika kutokana na uimara wa mpinzani wao Power Dynamos.


Ahmed amesema wanasikitika kumtoa mpinzani huyo ambaye laiti angepita, angekwenda kuongeza radha kwenye hatua inayofuata ya Makundi.


"Mpinzani alikuwa bora, lakini sisi tulikuwa bora zaidi yake ndio maana unaona alicheza vizuri lakini sisi tukamnyoa na tukamtupilia mbali. Tunasikitika kumtoa lakini sisi ni bora zaidi," alisema Ahmed.


Simba alimfurusha mpinzani wake huyo kwenye mchezo wa pili wa marudiano uliopigwa Oktoba Mosi, 2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar kwa kutoka sare ya 1-1 hivyo kupata faidi ya goli la ugenini ambapo yeye alimfunga Power Dynamos 2-2 nchini Zambia.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post