Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi amesema ratiba sio rafiki kwa sababu hakuna muda wa kufanya mazoezi hata hivyo kama kocha anafahamu ziko nyakati ratiba inaweza kuwa ngumu wanapaswa kuwa tayari kucheza wakati wowote
"Maandalizi kwa upande wetu siyo mazuri sana kutokana na ratiba lakini sisi ni wataalamu na ligi kuna muda inakuwa na ratiba ngumu lazima kuwa tayari. Leo tutakuwa na mazoezi jioni, ambayo yatatusaidia kuona hali ya wachezaji kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Geita Gold"
"Nafahamu kesho tutakuwa na mchezo mgumu na sijui hali ya Uwanja ikoje lakini nafikiri itakuwa kama Uwanja wa mchezo wetu uliopita. Ukweli nina wasiwasi sana na viwanja pamoja na maamuzi ya waamuzi uwanjani nina imani kutakuwa na mabadiliko kwenye hili kwasababu kila kitu kinaonekana wazi"
"Tumepoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu, lakini mashabiki wameendelea kuwa pamoja nasi na kutupa sapoti kama vile bado hatujapoteza mchezo wowote ni kazi yetu sasa kuhakikisha kwenye mchezo wa kesho tunajitoa kwa nguvu zote kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Gamondi
Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc juzi kwa kufungwa mabao 2-1, ni wazi Gamondi na vijana wake wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Geita Gold
Post a Comment