Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya kuwa nje kwa takribani miezi mitano akiuguza majeraha, mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula yuko tayari kuanza majukumu kwenye kikosi cha kwanza
Jana Simba ilirejea mazoezini Mo Simba Arena baada ya mapumziko ya siku chache Manula akiwa miongoni mwa wachezaji walioshiriki mazoezi hayo kikamilifu
Tanzania One amekamilisha program zote za mazoezi binafsi na sasa amejumuishwa kwenye mazoezi ya timu
Kama Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira ataridhishwa na utimamu wake wa mwili, anaweza kumtumia katika mchezo wa AFL dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa ijayo katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni wazi sasa mchezaji pekee ambaye bado ataendelea kukosekana ni Aubin Kramo kwani hata Hennock Inonga amepona na yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo
Post a Comment