Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Septemba 16 nchini Rwanda na mchezo wa marudiano kupigwa jijini Dar es salaam kati ya Septemba 28-30 katika uwanja wa Azam Complex
Ni dakika 180 za jasho na damu kwa Wananchi kuhakikisha wanamaliza ukame wa kutocheza makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa zaidi ya miaka 20
Aidha ni dakika 180 za kisasi dhidi ya Al Merrikh ambapo katika mechi zote za mtoano, Yanga haijawahi kuwatoa
Takwimu zinaonyesha timu hizo zilikutana hatua ya mtoano ligi ya mabingwa mwaka 1973, Al Merrikh wakishinda mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Tanzania na sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa huko Sudan
Katika mechi sita za mashindano ambazo timu hiyo zimekutana, mechi nne zilimalizika kwa matokeo ya sare huku Al Merrikh wakishinda mechi mbili
Yanga itakuwa ikisaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya wababe hao wa soka kutoka Sudan
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi pamoja na kuwa Yanga itakuwa na faida zaidi kwani Al Merrikh mchezo wao wa nyumbani hawatacheza kwao Sudan
Ni kutokana na machafuko yanayoendelea huko Sudan, Al Merrikh walitumia uwanja wa Pele, Kigali katika mchezo wao wa hatua ya awali
Jitihada za kuhamishia Morocco mchezo dhidi ya Yanga ziligonga mwamba na hivyo Al Merrikh kulazimika kubakia Rwanda
Kwa mazingira yanayowakabili Al Merrikh ni wazi Yanga ina kila sababu ya kupata matokeo ya ushindi na kusonga mbele hatua ya makundi
Yanga inaendelea na maandalizi chini ya kocha Miguel Gamondi kikosi kikitarajiwa kusafiri kwenda Rwanda Alhamisi, Septemba 14
Post a Comment