Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Jumamosi ya Septemba 16 2023, Yanga itakuwa ugenini nchini Rwanda kumenyama na El Merrikh katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema kutakuwa na 'session' za mazoezi mfululizo yaliyoandaliwa na Kocha Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi lengo likiwa kuhakikisha wanakuwa tayari kwa mchezo dhidi ya El Merrikh
Aidha Harrison amesema wanatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki wiki hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi
"Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki timu itaendelea na mazoezi Jumatatu (leo). Tutakuwa na session mbalimbali za mazoezi kwa kuzingatia mipango ya benchi la ufundi"
"Kwa muda tulionao, pengine tutacheza mechi moja ya kirafiki kabla ya timu kuelekea Rwanda tayari kwa mchezo," alisema Harrison
Habari njema kwa Gamondi ni kuwa baadhi ya wachezaji walio kwenye majukumu ya timu za Taifa watarejea mapema baada ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023
Nyota nane wa Yanga ambao wako na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wanatarajiwa kurejea kujiunga na wenzao baada ya mchezo dhidi ya Algeria utakaopigwa Alhamisi, Septemba 07
Post a Comment