Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Bodi ya Ligi Kuu imeupangia tarehe mchezo dhidi Namungo Fc ambao ulisogezwa mbele kupisha kalenda ya mashindano ya CAF na FIFA
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, mchezo huo utapigwa Septemba 20 katika uwanja wa Azam Complex
Hata hivyo tarehe hiyo inaweza kubadilika kama CAF itathibitisha uwepo wa mechi za mashindano ya CHAN yanayohusisha wachezaji wa ndani
Kulingana na kalenda ya CAF, mechi hizo zinapaswa kuanza mwishoni mwa mwezi Septemba 2023
Bodi pia imeipangia tarehe michezo mingine ambayo pia ilisogezwa mbele
Post a Comment