Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo huo wa mzunguuko wa tatu, utapigwa uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku
Itakuwa nafasi nzuri kwa Yanga kurejea juu katika msimamo wa ligi kama wataibuka na ushindi katika mchezo huo
Mashujaa Fc wako kileleni kwa muda baada ya kufikisha alama saba wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja
Aidha utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha msaidizi wa zamani wa Yanga Cedrick Kaze kukabiliana na waajiri wake hao wa zamani
Kaze ndiye mkufunzi wa Namungo ambapo mpaka sasa timu yake imeambulia alama moja kutoka mechi mbili walizocheza
Walifungwa na JKT Tanzania katika uwanja wao wa Majaliwa kabla ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na KMC katika uwanja huo huo
KMC na JKT Tanzania zote zilichapwa mabao 5-0 na Yanga katika mechi zao zilizofuata
Ni wazi utakuwa mchezo mgumu lakini malengo ya Kocha Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi ni kuona Wananchi wanaondoka na alama zote tatu ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi
Post a Comment