Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema timu itaondoka kwa usafiri wa ndege, kutakuwa na usafiri maalum wa mabasi kwa ajili ya mashabiki
Kamwe ametangaza gharama ya safari ya kwenda na kurudi Rwanda ni Tsh 150,000/- ambapo kwa shabiki atakayehitaji kusafiri lazima awe na hati ya kusafiria
"Msafara wetu utaondoka nchini Septemba 14, tuta safiri na mashabiki wengi na naamini tunaenda kuweka rekodi ya kujaza uwanja wa Pele, Rwanda"
"Mashabiki ni wengi wanaitaka hii safari, pia tuna mashabiki wa Yanga wapo Kigali.Tarehe 14 msafara wa mashabiki utaanza safari kutoka Dar - Kigali saa 11 alfajiri na tutalala Kahama"
"Gharama ya safari ni TSH 150,000/- na mashabiki anapaswa kuwa na hati ya kusafiria au kibali cha safari," alisema Kamwe
Akizungumzia maandalizi ya kikosi, Kamwe amesema timu imerejea mazoezini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki
Siku ya Jumapili Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ambayo itatangazwa baadae. Hata hivyo amesema Yanga inatoa mwaliko kwa timu yoyote ambayo inataka kujipima na Yanga katika uwanja wowote
"Tunatarajia kuwa na mchezo wa kirafiki siku ya jumapili. Tutatangaza tunacheza na timu gani. Hata hivyo tunatoa fursa kwa timu yoyote inaweza kuomba mchezo wa kirafiki na sisi tutacheza popote pale"
Post a Comment