Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Jumamosi ijayo, Septemba 16 Yanga itakuwa Rwanda kuchuana na AL Merrikh katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Miguel Gamondi alitoa mapumziko kwa siku ya leo Jumapili
Aidha Kamwe amesema Yanga inafanya utaratibu wa kumsafiri kiungo Stephane Aziz Ki ambaye yuko Morocco na timu ya Taifa ya Burkina Faso
"Kocha (Gamondi) alitoa mapumziko kwa wachezaji wote siku ya leo hivyo tunatarajiwa hapo kesho wote ikiwa ni pamoja na wale waliokuwa katika majukumu ya timu ya Taifa wataripoti mazoezini"
"Kuhusu kiungo wetu Stephane Aziz Ki ambaye yuko Morocco ambako walipaswa kucheza dhidi ya Morocco lakini mchezo huo umeahirishwa kutokana na tetemeko la arhi lililokumba nchi hiyo"
"Tumewasiliana nae, yuko salama na wachezaji wenzake wa Burkina Faso, uongozi umewasiliana na FA ya Burkina Faso na tunaandaa utaratibu kuhakikisha Aziz Ki anarejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Merrikh," alisema Kamwe
Post a Comment