Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ni katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh
Kamwe amesema msimu huu Yanga iliweka malengo ya kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa na wamebakisha dakika 90 kuhakikisha wanakamilisha malengo
Kamwe ametamba kuwa Azam Complex utaweka rekodi mpya ya kuingiza mashabiki wengi katika siku hiyo ambayo wataifanya kuwa maalum kwa Wananchi
"Tuliweka wazi mapema, Lengo letu namba moja Wananchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Msimu huu ni kucheza hatua ya Makundi"
"Mpaka sasa kwa asimilia 50 lengo letu linaelekea kutimia. Tuna Faida mkononi mwetu ya magoli 2-0 tuliyoyapata Ugenini. Kazi imebaki nyumbani"
"Klabu namba tatu kwa ubora wa Afrika kumalizana na Al Merrikh na kutimiza lengo letu. Ni Jumamosi ya kishindo kipya cha Wananchi. Jumamosi ambayo Afrika inatakiwa ilishuhudie Jeshi la kijani na njano kikifanya balaa lake"
"Jumamosi ambayo uwanja wa Azam Complex utaandika Rekodi mpya ya kupokea mashabiki wengi zaidi katika Historia yake tangu ulipozinduliwa," alitamba Kamwe
Post a Comment